Kwa mujibu wa Shirika la Habari Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa idadi ya waathirika waliopoteza maisha kutokana na njaa na utapiamlo imefikia watu 453, wakiwemo watoto 150.
Takwimu hizi zimeongezeka tangu kutangazwa rasmi kwa baa la njaa na faharasa ya IPC. Katika siku chache zilizopita pekee, vifo 175 vipya vimeripotiwa, vikiwemo watoto 35.
Wakati hali hii ya kibinadamu ikizidi kuwa mbaya, mashambulizi ya anga na mizinga ya Israel dhidi ya maeneo mbalimbali ya Gaza yanaendelea. Katika shambulizi karibu na mhimili wa Netsarim, mtoto mmoja aliuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa. Kadhalika, katika shambulizi magharibi mwa Deir al-Balah, mama mmoja na watoto wake sita waliuwawa. Maeneo mengine kama kambi ya al-Shati, al-Zawaida, Khan Younis na mashariki mwa Deir al-Balah pia yamelengwa.
Ripoti zinaonyesha kuwa ndege zisizo na rubani za Israel zimerusha mabomu ya gesi kwenye nyumba karibu na Hospitali
Your Comment